Home / GOSSIP / Licha ya kufanya kazi pamoja ndani ya WCB, Rayvanny amfananisha hivi Diamond Platnumz

Licha ya kufanya kazi pamoja ndani ya WCB, Rayvanny amfananisha hivi Diamond Platnumz

 

Msanii kutoka WCB Wasafi Raymond a.k.a Rayvanny amefunguka na kusema kuwa vitu vyenye majina mengi siku zote huwa ni hatari sana hivyo hata yeye anashindwa kumuelezea Diamond Platnumz kutokana na moyo wake wa upendo na kujali.

Rayvanny alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz na kudai kuwa yeye anamkubali sana Diamond Platnumz kwa sababu kwanza ni mtu mwenye moyo wa upendo lakini pia msanii huyo anakumbuka kuna Mungu na pia anakumbuka kuwa kuna kifo ndiyo maana anakuwa anajitoa sana kwa watu na jamii.

rayvanny-20161011-0002

”Mungu ana majina mengi sana, Jehova, Mfalme, Mungu wa miungu, Baba wa watu wote halafu pesa pia ina majina mengi sana Pesa, Ankara, Mshiko, Money, Michakato sijui Njere halafu pia Diamond Platnumz ana majina mengi pia sijui Chibu, Dangote, Chibu D, Simba, Toto la Kimanyema so vitu vyenye majina mengi ni hatari sana”.

Rayvanny akaendelea kwa kumuelezea Diamond namna hii: “Kwa hiyo ukiniambia Diamond namuonaje mwenyewe nashindwa kumuelezea sababu kwanza ni mtu mwenye moyo wa ubinadamu, ana moyo wa kukumbuka kama kuna Mungu, kuna kifo ndiyo maana unaweza kumuona kwenye vituo vya watoto yatima anawasaidia, anasaidia vijana wengi ambao wana vipaji anawapa watu fursa, hivyo ni mtu ambaye amefunguliwa na Mungu njia zake ndiyo maana unaweza kuona ana majina mengi na hapo nimekutajia baadhi ya vitu vyenye majina mengi ili uone siri ya vitu vyenye majina mengi vinakuaje”

Comments

comments

Check Also

DIAMOND PLATINUMS STATEMENT AFTER HARMONIZE

DiamondplatnumzI remember last year you came to receive me at the airport when I was …

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.